1 Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, katika habari za Wafilisti, kabla Farao hajapiga Gaza. 2:4-7; Zek 9:5-7
2 BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi watapiga yowe.
3 Kwa sababu ya mshindo wa kukanyaga kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbiombio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya ngurumo ya magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;
4 kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
5 Upaa umeupata Gaza;Ashkeloni umenyamazishwaMabaki ya bonde lao;Hata lini utajikata-kata?
6 Ee upanga wa BWANA,Siku ngapi zitapita kabla hujatulia?Ujitie katika ala yako;Pumzika, utulie.
7 Utawezaje kutulia,Ikiwa BWANA amekupa agizo?Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani,Ndipo alipoyaamuru hayo.