14 Mwasemaje ninyi, Sisi tu mashujaa, watu hodari wa vita.
15 Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wametelemka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.
16 Msiba wa Moabu umefika karibu,Na mateso yake yanafanya haraka.
17 Ninyi nyote mnaomzunguka, mlilieni,Nanyi nyote mlijuao jina lake, semeni,Jinsi ilivyovunjika fimbo ya enzi,Fimbo ile iliyokuwa nzuri!
18 Ee binti ukaaye Diboni,Shuka toka utukufu wako, ukae katika kiu;Maana atekaye Moabu amepanda juu yako,Ameziharibu ngome zako.
19 Wewe ukaaye Aroeri,Simama kando ya njia upeleleze;Mwulize mwanamume akimbiaye na mwanamke atorokaye,Sema, Imetendeka nini?
20 Moabu ameaibishwa, kwa maana amevunjika;Pigeni yowe na kulia;Tangazeni habari hii katika Arnoni,Ya kuwa Moabu ameharibika.