21 Na hukumu imeifikilia nchi tambarare; juu ya Holoni, na juu ya Yasa, na juu ya Mefaathi;
22 na juu ya Diboni, na juu ya Nebo, na juu ya Beth-diblathaimu;
23 na juu ya Kiriathaimu, na juu ya Beth-gamuli, na juu ya Beth-meoni;
24 na juu ya Keriothi, na juu ya Bozra, na juu ya miji yote ya nchi ya Moabu, iliyo mbali na iliyo karibu.
25 Pembe ya Moabu imekatika, na mkono wake umevunjika, asema BWANA. Mlevyeni; kwa maana alijitukuza juu ya BWANA
26 na Moabu atagaa-gaa katika matapiko yake, naye atadhihakiwa. Kwa maana Israeli, je! Hakuwa dhihaka kwako?
27 Alionekana kati ya wevi? Maana kila umtajapo watikisa kichwa chako.