35 Udhalimu niliotendwa mimi, na uliotendwa mwili wangu, umpate Babeli; ndivyo atakavyosema yeye akaaye Sayuni; na Yerusalemu atasema, Damu yangu na iwe juu yao wakaao katika Ukaldayo.
36 Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu.
37 Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwa-mwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.
38 Watanguruma pamoja kama wana-simba; watanguruma kama simba wachanga.
39 Wakiingiwa na ukali, nitawafanyizia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA.
40 Nitawatelemsha kama wana-kondoo machinjoni, kama kondoo waume pamoja na mabeberu.
41 Jinsi Sheshaki alivyotwaliwa!Naye sifa ya dunia yote alivyoshambuliwa!Jinsi Babeli alivyokuwa ukiwaKatikati ya mataifa!