37 Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwa-mwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.
38 Watanguruma pamoja kama wana-simba; watanguruma kama simba wachanga.
39 Wakiingiwa na ukali, nitawafanyizia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA.
40 Nitawatelemsha kama wana-kondoo machinjoni, kama kondoo waume pamoja na mabeberu.
41 Jinsi Sheshaki alivyotwaliwa!Naye sifa ya dunia yote alivyoshambuliwa!Jinsi Babeli alivyokuwa ukiwaKatikati ya mataifa!
42 Bahari imefika juu ya Babeli,Umefunikwa kwa wingi wa mawimbi yake.
43 Miji yake imekuwa maganjo;Nchi ya ukame, na jangwa;Nchi asimokaa mtu ye yote,Wala hapiti mwanadamu huko.