28 Huo ndio urithi wa wana wa Gadi sawasawa na jamaa zao, miji yake na vijiji vyake.
29 Kisha Musa akawapa hao wa nusu ya kabila ya Manase urithi wao; ulikuwa ni wa hiyo nusu ya kabila ya wana wa Manase sawasawa na jamaa zao.
30 Na mpaka wao ulikuwa kutoka huko Mahanaimu, Bashani yote, na ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini;
31 na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase maana, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao.
32 Hizi ndizo mirathi ambazo Musa alizigawanya katika nchi tambarare za Moabu, ng’ambo ya pili ya Yordani, kukabili Yeriko, upande wa mashariki.
33 Lakini Musa hakuwapa kabila ya Lawi urithi uwao wote; yeye BWANA, Mungu wa Israeli, ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.