5 Kwa maana dhambi zake zimekuwa nyingi mno,zimerundikana mpaka mbinguni,na Mungu ameyakumbuka maovu yake.
6 Mtendeeni kama alivyowatendea nyinyi;mlipeni mara mbili kwa yale aliyoyatenda.Mchanganyieni kikombeni mwake kinywaji kikali maradufu.
7 Mpeni mateso na uchungu kadiri ya kujigamba kwake,kulingana na kuishi kwake kwa anasa.Maana anajisemea moyoni: ‘Ninaketi hapa; mimi ni malkia.Mimi si mjane, wala sitapatwa na uchungu!’
8 Kwa sababu hiyo mabaa yake yatampata kwa siku moja:Ugonjwa, huzuni na njaa.Atachomwa moto,maana Bwana Mungu mwenye kumhukumu ana nguvu.”
9 Wafalme wa dunia waliofanya uzinzi naye na kuishi naye maisha ya anasa wataomboleza na kulia wakati watakapoona moshi wa mji huo unaoteketea.
10 Wanasimama kwa mbali kwa sababu ya kuogopa mateso yake na kusema, “Ole! Ole kwako Babuloni, mji maarufu na wenye nguvu! Kwa muda wa saa moja tu adhabu yako imekupata.”
11 Wafanyabiashara wa dunia watalia na kumfanyia matanga, maana hakuna mtu anayenunua tena bidhaa zao;