7 Maana kama lile agano la kwanza halingalikuwa na dosari, hakungalikuwa na haja ya agano la pili.
8 Lakini Mungu aliwalaumu watu wake aliposema:“Siku zinakuja, asema Bwana,ambapo nitafanya agano jipyana watu wa Israeli na wa Yuda.
9 Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na babu zaosiku nilipowaongoza kwa mkono kutoka Misri.Hawakuwa waaminifu kwa agano langu;na hivyo mimi sikuwajali, asema Bwana.
10 Hili ndilo agano nitakalofanya na watu wa Israeli siku zijazo, asema Bwana:Nitaweka sheria zangu akilini mwao,na kuziandika mioyoni mwao.Mimi nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu.
11 Hakuna atakayemfundisha mwananchi mwenzake,wala atakayemwambia ndugu yake:‘Mjue Bwana’.Maana wote, wadogo na wakubwa, watanijua mimi.
12 Nitawasamehe makosa yao,wala sitakumbuka tena dhambi zao.”
13 Kwa kusema juu ya agano jipya, Mungu alilichakaza lile la kwanza; na chochote kinachochakaa na kuwa kikuukuu kitatoweka karibuni.