1 “Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyanganyi.
2 Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo.
3 Mngojamlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake, na kuwaongoza nje.
4 Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake.
5 Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.”
6 Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.
7 Basi, akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo.