34 Nawapeni amri mpya: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi.
35 Mkipendana, watu wote watajua kwamba nyinyi ni wanafunzi wangu.”
36 Simoni Petro akamwuliza, “Bwana, unakwenda wapi?” Yesu akajibu, “Niendako huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.”
37 Petro akamwambia “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Niko tayari kufa kwa ajili yako!”
38 Yesu akajibu, “Je, uko tayari kweli kufa kwa ajili yangu? Kweli nakuambia, kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu!”