3 Yaredi akamzaa Henoki, Henoki akamzaa Methusela. Methusela alimzaa Lameki,
4 Lameki akamzaa Noa. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.
5 Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
6 Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Difathi na Togama.
7 Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.
8 Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani.
9 Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.