1 Hayo ndiyo makundi ya wazawa wa Aroni. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
2 Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakawa makuhani.
3 Mfalme Daudi aliwapanga wazawa wa Aroni katika makundi kufuatana na huduma zao. Alisaidiwa kufanya hivyo na Sadoki, mzawa wa Eleazari, na Ahimeleki, mzawa wa Ithamari.
4 Kwa vile ambavyo kulipatikana viongozi wanaume wengi zaidi miongoni mwa wazawa wa Ithamari, waliwagawanya wazawa wa Eleazari chini ya viongozi kumi na sita, na wazawa wa Ithamari chini ya viongozi wanane.
5 Waligawanywa kwa kura kwani kulikuwa na wakuu wa mahali patakatifu na viongozi wa kidini miongoni mwa koo zote mbili, yaani ukoo wa Eleazari na ukoo wa Ithamari.
6 Naye Shemaya mwana wa Nathaneli, mwandishi, aliyekuwa Mlawi, aliwaandika mbele ya mfalme Daudi, maofisa wake, kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi. Ukoo wa Eleazari ulipata kura mbili, na ukoo wa Ithamari kura moja.
7 Kura ya 1 ilimwangukia Yoaribu; ya 2 Yedaya;
8 ya 3 Harimu; ya 4 Seorimu;
9 ya 5 Malkia; ya 6 Miyamini;
10 ya 7 Hakosi; ya 8 Abiya;
11 ya 9 Yeshua; ya 10 Shekania;
12 ya 11 Eliashibu; ya 12 Yakimu;
13 ya 13 Hupa; ya 14 Yeshebeabu;
14 ya 15 Bilga; ya 16 Imeri;
15 ya 17 Heziri; ya 18 Hapisesi;
16 ya 19 Pethahia; ya 20 Yehezkeli;
17 ya 21 Yakini; ya 22 Gamuli;
18 ya 23 Delaya; na ya 24 Maazia.
19 Hawa waliandikishwa kulingana na kazi zao kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kutoa huduma, kadiri ya utaratibu waliowekewa na Aroni babu yao, kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
20 Hawa ndio wazawa wengine wa Lawi: Mmoja wa wazawa wa Amramu alikuwa Shubaeli; wa Shubaeli alikuwa Yedeya.
21 Mmoja wa wazawa wa Rehabia alikuwa Ishio kiongozi wa ukoo.
22 Mmoja wa wazawa wa Ishio alikuwa Shelomithi na wa wazawa wa Shelomithi alikuwa Yahathi.
23 Wana wa Hebroni walikuwa: Yeria wa kwanza, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yakameamu wa nne.
24 Mmoja wa wana wa Uzieli alikuwa Mika. Mmoja wa wazawa wa Mika alikuwa Shamire.
25 Mmoja wa wazawa wa Ishia nduguye Mika alikuwa Zekaria.
26 Wana wa Merari: Mahli, Mushi na Yaazia;
27 wazawa wa Merari kwa mwanawe Yaazia: Shohamu, Zakuri na Ibri.
28 Wana wa Mahli: Eleazari ambaye hakupata mtoto,
29 Kishi ambaye alikuwa na mwana mmoja: Yerameeli.
30 Mushi alikuwa na wana watatu: Mahli, Ederi na Yeremothi. Wao ni wazawa wa Lawi kulingana na koo zao.
31 Pia hao wote walipiga kura kufuatana na ukoo wa kila mkuu na mdogo wake, kama wazawa wa Aroni walivyofanya. Walipiga kura mbele ya mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi.