1 Hawa ndio wana wa mfalme Daudi waliozaliwa wakati alipokuwa huko Hebroni:Amnoni, mzaliwa wake wa kwanza; mama yake aliitwa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili, Mkarmeli;
2 wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, bintiye Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne alikuwa Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;
3 wa tano alikuwa Shefatia, ambaye mama yake alikuwa Abitali; na wa sita alikuwa Ithreamu, ambaye mama yake alikuwa Egla.
4 Wote sita, walizaliwa Hebroni ambako Daudi alitawala kwa muda wa miaka saba na nusu. Huko Yerusalemu, alitawala kwa muda wa miaka thelathini na mitatu.
5 Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni.
6 Na mbali na hao alikuwa na wana wengine tisa: Ibhari, Elishua, Elifaleti,
7 Noga, Nefegi, Yafia,
8 Elishama, Eliada na Elifeleti.
9 Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wengine waliozaliwa na masuria wake. Daudi alikuwa na binti pia, aliyeitwa Tamari.
10 Wazawa wa mfalme Solomoni: Solomoni alimzaa Rehoboamu, aliyemzaa Abiya, aliyemzaa Asa, aliyemzaa Yehoshafati,
11 aliyemzaa Yehoramu, aliyemzaa Ahazia, aliyemzaa Yoashi,
12 aliyemzaa Amazia, aliyemzaa Uzia, aliyemzaa Yothamu,
13 aliyemzaa Ahazi, aliyemzaa Hezekia, aliyemzaa Manase,
14 aliyemzaa Amoni, aliyemzaa Yosia.
15 Yosia alikuwa na wana wanne: Yohanani, mzaliwa wake wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia na wa nne Shalumu.
16 Yehoyakimu alikuwa na wana wawili: Yekonia na Sedekia.
17 Wana wa Yekonia aliyechukuliwa mateka na Wababuloni walikuwa saba: Shealtieli,
18 Malkiramu, Pedaya, Shenazari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.
19 Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Zerubabeli alikuwa na wana wawili: Meshulamu na Hanania, na binti mmoja, jina lake Shelomithi.
20 Zerubabeli pia alikuwa na wana wengine watano: Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-hesedi.
21 Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Yeshaya alimzaa Refaya, aliyemzaa Arnani, aliyemzaa Obadia, aliyemzaa Shekania.
22 Shekania alimzaa Shemaya. Wana wa Shemaya walikuwa sita: Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati.
23 Nearia alikuwa na wana watatu: Eliehonai, Hizkia na Azrikamu.
24 Eliehonai alikuwa na wana saba: Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani.