36 Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna na Amaleki.
37 Wana wa Reueli walikuwa Nahathi, Zera, Shama na Miza.
38 Wana wa Seiri walikuwa Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.
39 Wana wa Lotani walikuwa wawili: Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.
40 Wana wa Shobali walikuwa Alvani, Manahathi, Ebali, Shefi na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa Aya na Ana.
41 Mwana wa Ana alikuwa Dishoni; na wana wa Dishoni walikuwa Hamrani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
42 Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani na Akani; na wana wa Dishoni walikuwa Usi na Arani.