6 Zera nduguye alikuwa na wana watano: Zimri, Etheni, Hemani, Kalkoli na Dara.
7 Mwana wa Karmi, alikuwa Akari. Huyu aliwaletea Waisraeli taabu kwa sababu alijiwekea nyara zilizokuwa zimewekwa wakfu.
8 Ethani alikuwa na mwana mmoja, jina lake Azaria.
9 Wana wa Hesroni walikuwa Yerameeli, Ramu na Kelubai.
10 Ramu alimzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa kabila la Yuda.
11 Nashoni alimzaa Salma, Salma akamzaa Boazi,
12 Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.