9 Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wengine waliozaliwa na masuria wake. Daudi alikuwa na binti pia, aliyeitwa Tamari.
10 Wazawa wa mfalme Solomoni: Solomoni alimzaa Rehoboamu, aliyemzaa Abiya, aliyemzaa Asa, aliyemzaa Yehoshafati,
11 aliyemzaa Yehoramu, aliyemzaa Ahazia, aliyemzaa Yoashi,
12 aliyemzaa Amazia, aliyemzaa Uzia, aliyemzaa Yothamu,
13 aliyemzaa Ahazi, aliyemzaa Hezekia, aliyemzaa Manase,
14 aliyemzaa Amoni, aliyemzaa Yosia.
15 Yosia alikuwa na wana wanne: Yohanani, mzaliwa wake wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia na wa nne Shalumu.