25 Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu; Shalumu alimzaa Mibsamu na Mibsamu akamzaa Mishma.
26 Mishma alimzaa Hamueli, aliyemzaa Zakuri, na Zakuri akamzaa Shimei.
27 Shimei alikuwa na wana kumi na sita na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na wana wengi, na jamii yake pia haikuongezeka kama kabila la Yuda.
28 Miji walimokuwa wakiishi ilikuwa Beer-sheba, Molada, Hasar-shuali,
29 Bilha, Ezemu, Toladi;
30 Bethueli, Horma, Siklagi,
31 Beth-markabothi, Hazar-susimu, Beth-biri na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao mpaka wakati wa utawala wa mfalme Daudi.