16 Waliishi katika sehemu ya Gileadi, katika Bashani na miji yake na katika malisho yote ya Sharoni, hadi mipakani.
17 Watu hao wote waliandikishwa katika koo, katika siku za Yothamu, mfalme wa Yuda, na Yeroboamu, mfalme wa Israeli.
18 Makabila ya Reubeni, Gadi na Manase ya mashariki, yalikuwa na wanajeshi shupavu wapatao 44,760, wenye ngao na mapanga, wavuta pinde stadi vitani.
19 Walipigana vita na makabila ya Wahajiri, Yeturi, Nafishi na Nodabu.
20 Waliweka tumaini lao kwa Mungu na wakamwomba awasaidie, naye akaitikia ombi lao na kuwatia mikononi mwao Wahajiri pamoja na marafiki zao.
21 Waliteka nyara ngamia 50,000, kondoo 250,000, punda 2,000 na mateka hai 100,000.
22 Waliua maadui wengi sana kwa sababu vita hivyo vilikuwa ni vita vya Mungu. Nao waliendelea kuishi katika nchi hiyo, mpaka wakati wa uhamisho.