21 Zabadi na Shuthela. Mbali na Shuthela, Efraimu alikuwa na wana wengine wawili, Ezeri, na Eleadi, ambao waliuawa na wenyeji wa asili wa nchi ya Gathi kwa sababu walikwenda huko kuwanyanganya mifugo yao.
22 Efraimu baba yao aliomboleza vifo vyao kwa siku nyingi sana, na ndugu zake wakaja kumfariji.
23 Ndipo Efraimu akalala na mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana. Efraimu akampa jina Beria, kwa sababu ya maafa yaliyoipata jamaa yake.
24 Efraimu alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliyeijenga miji ya Beth-horoni ya juu na chini, na Uzen-sheera.
25 Efraimu alimzaa pia Refa ambaye alimzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,
26 Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama,
27 Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua.