36 Wana wa Sofa walikuwa Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra,
37 Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera.
38 Wana wa Yetheri walikuwa Yefune, Pispa na Ara.
39 Wana wa Ula walikuwa Ara, Hanieli na Risia.
40 Hao wote walikuwa wazawa wa Asheri na walikuwa wakuu wa jamaa zao, watu wateule na hodari wa vita. Idadi ya wale walioandikishwa kwa kufuata koo katika jeshi ilikuwa 26,000.