10 Shelomithi, mwana wa Yosifia, wa ukoo wa Bani, pamoja na wanaume 160.
11 Zekaria, mwana wa Bebai, wa ukoo wa Bebai, pamoja na wanaume 28.
12 Yohanani, mwana wa Hakatani, wa ukoo wa Azgadi, pamoja na watu 110.
13 Elifeleti, Yeueli na Shemaya, wa ukoo wa Adonikamu, pamoja na wanaume 60, (hawa walirudi baadaye).
14 Uthai na Zakuri, wa ukoo wa Bigwai, pamoja na wanaume 70.
15 Niliwakusanya pamoja watu wote kando ya mto uelekeao mji wa Ahava. Huko, tulipiga kambi kwa muda wa siku tatu. Niliwakagua watu wote pamoja na makuhani, lakini sikupata Walawi miongoni mwao.
16 Niliita waje kwangu viongozi tisa: Eliezeri, Arieli, Shemaya, Elnathani, Yaribu, Elnathani, Nathani, Zekaria na Meshulamu, pamoja na waalimu wawili, Yoyaribu na Elnathani.