18 Juu ya kabila la Zebuluni na kabila la Isakari, alisema,“Zebuluni, furahi katika safari zako;nawe Isakari, furahi katika mahema yako.
19 Watawaalika wageni kwenye milima yao,na huko watu watatoa sadaka zinazotakiwa.Maana wao watapata utajiri wao kutoka baharinina hazina zao katika mchanga wa pwani.”
20 Juu ya kabila la Gadi, alisema:“Atukuzwe Mungu ampatiaye Gadi sehemu kubwa.Gadi hunyemelea kama simbaakwanyue mkono na utosi wa kichwa.
21 Alijichagulia eneo zuri kuliko yote,mahali ilipotengwa sehemu ya kiongozi.Aliwaongoza watu na kumtii Mwenyezi-Mungu,alitekeleza mpango wa Mungu kwa Israeli.”
22 Juu ya kabila la Dani alisema hivi:“Dani ni mwanasimbaarukaye kutoka Bashani.”
23 Juu ya kabila la Naftali alisema:“Ee Naftali fadhili,uliyejaa baraka za Mwenyezi-Mungu,nchi yako ni kusini kwenye ziwa Kinerethi.”
24 Juu ya kabila la Asheri alisema:“Asheri abarikiwe kuliko watoto wote wa Yakobo,na upendelewe na ndugu zako wote;na achovye mguu wake katika mafuta.