7 Juu ya kabila la Yuda alisema:“Ee Mwenyezi-Mungu usikilize kilio cha kabila la Yuda;umrudishe tena kwa watu wale wengine.Upigane kwa mikono yako kwa ajili yake,ulisaidie kabila la Yuda dhidi ya adui zake.”
8 Juu ya kabila la Lawi, alisema:“Ee Mwenyezi-Mungu ulipatie Lawi kauli yako ya Urimu,kauli yako ya thumimu kwa hao waaminifu wako,ambao uliwajaribu huko Masa.
9 Ulishindana nao kwenye maji ya Meriba.Walawi walioamua kuwaacha wazee wao,wakawasahau jamaa zao,wasiwatambue hata watoto waomaana walizingatia amri zako,na kushika agano lako.
10 Na wawafundishe wazawa wa Yakobo maagizo yako;wawafundishe watu wa Israeli sheria yako.Walawi na wafukize ubani mbele yako,sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni pako.
11 Ee Mwenyezi-Mungu, uzibariki nguvu zao,uzikubali kazi za mikono yao;uzivunjilie mbali nguvu za maadui zao,nguvu za wanaowachukia hata wasiinuke tena.”
12 Juu ya kabila la Benyamini alisema:“Hili ni kabila alipendalo Mwenyezi-Mungu,nalo hukaa salama karibu naye.Yeye hulilinda mchana kutwa,na kukaa kati ya milima yake.”
13 Juu ya kabila la Yosefu alisema:“Mwenyezi-Mungu na aibariki nchi yake,kwa baraka nzuri kabisa kutoka juu,