6 Watu wangu wamepata adhabu kubwakuliko watu wa mji wa Sodomamji ambao uliteketezwa ghaflabila kuwa na muda wa kunyosha mkono.
7 Vijana wa Siyoni walikuwa safi kuliko theluji,walikuwa weupe kuliko maziwa.Miili yao ilikuwa myekundu kama matumbawe,uzuri wa viwiliwili vyao kama johari ya rangi ya samawati.
8 Sasa sura zao ni nyeusi kuliko makaa,wanapita barabarani bila kujulikana;ngozi yao imegandamana na mifupa yaoimekauka, imekuwa kama kuni.
9 Afadhali waliouawa kwa upangakuliko waliokufa kwa njaa,ambao walikufa polepolekwa kukosa chakula.
10 Kina mama ambao huwa na huruma kuuwaliwapika watoto wao wenyewe,wakawafanya kuwa chakula chaowakati watu wangu walipoangamizwa.
11 Mwenyezi-Mungu alionesha uzito wa ghadhabu yake,aliimimina hasira yake kali;aliwasha moto huko mjini Siyoniambao uliteketeza misingi yake.
12 Wafalme duniani hawakuaminiwala wakazi wowote wa ulimwenguni,kwamba mvamizi au aduiangeweza kuingia malango ya Yerusalemu.