1 Kisha nikaona udhalimu wote unaofanyika duniani. Watu wanaokandamizwa hulia machozi, lakini hakuna yeyote anayewafariji. Wakandamizaji wao wana nguvu, ndiyo sababu hakuna wa kuwafariji.
2 Basi, nikafikiri moyoni kuwa wafu waliokwenda wasikorudi, wana nafuu zaidi kuliko watu walio hai.
3 Lakini ana heri zaidi kuliko wafu na walio hai, yule ambaye bado hajazaliwa na kuona maovu yote yanayotendwa hapa duniani.
4 Tena niligundua kwamba juhudi zote za mtu na ujuzi wake katika kazi vyatokana na kuoneana wivu. Hayo nayo ni bure kabisa; ni sawa na kufukuza upepo.
5 Mpumbavu hafanyi kazina mwisho hujiua kwa njaa.
6 Ni afadhali kuwa na kidogo tu, pamoja na amani moyoni,kuliko kuwa na mengi, pamoja na taabu;sawa tu na kufukuza upepo.
7 Tena, niliona jambo moja bure kabisa duniani.