10 Enyi watu wa Siyoni,lieni na kugaagaa kama mama anayejifungua!Maana sasa mtaondoka katika mji huumwende kukaa nyikani,mtakwenda mpaka Babuloni.Lakini huko, mtaokolewa.Huko Mwenyezi-Mungu atawakomboa makuchani mwa adui zenu.
11 Mataifa mengi yamekusanyika kuwashambulia.Yanasema: “Acheni mji wao utiwe najisi,nasi tuyaone magofu ya Siyoni!”
12 Lakini waohawafahamu mawazo ya Mwenyezi-Munguwala hawaelewi mpango wake:Kwamba amewakusanya pamoja,kama miganda mahali pa kupuria.
13 Mwenyezi-Mungu asema,“Enyi watu wa Siyoni,inukeni mkawaadhibu adui zenu!Nitawapeni nguvu kama fahalimwenye pembe za chuma na kwato za shaba.Mtawasaga watu wa mataifa mengi;mapato yao mtaniwekea wakfu mimi,mali zao mtanitolea mimi Bwana wa dunia yote.”