1 Jumuikeni mkajikusanye enyi watu wa Yerusalemu;mkisema: “Tumezingirwa, tumesongwa;naye kiongozi wa Israeli wanampiga shavuni kwa fimbo.”
2 Mwenyezi-Mungu asema,“Lakini wewe Bethlehemu katika Efratha,wewe ni mdogo tu kati ya jamii za Yuda,lakini kwako kutatoka mtawalaatakayetawala juu ya Israeli kwa niaba yangu.Asili yake ni ya zama za kale.”
3 Hivyo Mungu atawaacha watu wake kwa maadui,mpaka yule mama mjamzito atakapojifungua.Kisha ndugu zake waliobakia,watarudi na kuungana na Waisraeli wenzao.
4 Huyo mtawala atawachunga watu wake kwa nguvu ya Mwenyezi-Mungu,kwa fahari yake Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.Watu wake wataishi kwa usalama,maana atakuwa mkuu mpaka miisho ya dunia.