9 Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu?Yeye atawakomesha na kuwaangamiza,wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.
10 Watateketezwa kama kichaka cha miiba,kama vile nyasi zilizokauka.
11 Kwako kumetoka aliyepanga maovu dhidi ya Mwenyezi-Mungualiyefanya njama za ulaghai.
12 Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake:“Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu,wao wataangushwa na kuangamizwa.Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu,sitawateseni tena zaidi.
13 Sasa nitaivunja nira ya Ashuru shingoni mwenu,na minyororo waliyowafungia nitaikatakata.”
14 Mwenyezi-Mungu ameamuru hivi kuhusu Ninewi:“Hutapata wazawa kulidumisha jina lako.Sanamu zako za kuchonga na za kusubu,nitazivunjavunja nyumbani mwa miungu yako.Mimi nitakuchimbia kaburi lako,maana wewe hufai kitu chochote.”
15 Enyi watu wa Yuda tazameni:Anakuja kutoka mlimani mtu anayeleta habari njema,mjumbe ambaye anatangaza amani.Adhimisheni sikukuu zenu, enyi watu wa Yuda,timizeni nadhiri zenu,maana waovu hawatawavamia tena,kwani wameangamizwa kabisa.