4 Ido, Ginethoni, Abiya,
5 Miyamini, Maadia, Bilga,
6 Shemaya, Yoyaribu, Yedaya,
7 Salu, Amoki, Hilkia na Yedaya. Hao walikuwa ni wakuu wa makuhani na ndugu zao wakati wa Yeshua.
8 Walawi: Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda na Matania, ambaye alihusika na usimamizi wa nyimbo za shukrani akishirikiana na ndugu zake.
9 Nao Bakbukia na Uno rafiki zao, walisimama ibadani mkabala nao.
10 Yeshua alimzaa Yoyakimu, Yoyakimu alimzaa Eliashibu, Eliashibu alimzaa Yoyada,