61 Watu wa miji ifuatayo, nao walirudi: Wa Tel-mela, wa Tel-harsha, wa Kerubu, wa Adoni na wa Imeri; ila haikuwezekana kuthibitisha kama walikuwa wazawa wa Waisraeli
62 wazawa wa Delaya, Tobia na wa Nekoda; jumla: Watu 642.
63 Wazawa wa koo zifuatazo za makuhani pia walirudi: Ukoo wa Hobaya, wa Hakozi na wa Barzilai (aliyekuwa ameoa binti za Barzilai, Mgileadi, naye akachukua jina la ukoo huo).
64 Hao walitafuta orodha yao kati ya wengine walioorodheshwa katika kumbukumbu za koo, lakini ukoo wao haukuwemo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika huduma ya ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi.
65 Mtawala akawaambia kuwa hawaruhusiwi kushiriki chakula kitakatifu sana, mpaka afike kuhani mwenye kauli ya Urimu na Thumimu.
66 Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni jumla yao ilikuwa 42,360.
67 Tena kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7,337, nao walikuwa waimbaji wanaume na wanawake, wote 245.