64 Hao walitafuta orodha yao kati ya wengine walioorodheshwa katika kumbukumbu za koo, lakini ukoo wao haukuwemo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika huduma ya ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi.
65 Mtawala akawaambia kuwa hawaruhusiwi kushiriki chakula kitakatifu sana, mpaka afike kuhani mwenye kauli ya Urimu na Thumimu.
66 Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni jumla yao ilikuwa 42,360.
67 Tena kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7,337, nao walikuwa waimbaji wanaume na wanawake, wote 245.
68 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,
69 ngamia 435, na punda 6,720.
70 Baadhi ya wakuu wa koo walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala wa mkoa alitoa kilo 8 za dhahabu, mabirika 50, mavazi 530.