70 Baadhi ya wakuu wa koo walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala wa mkoa alitoa kilo 8 za dhahabu, mabirika 50, mavazi 530.
71 Baadhi ya wakuu wa koo walitoa kilo 168 za dhahabu, na kilo 1,250 za fedha.
72 Matoleo ya watu wengine wote yalikuwa kilo 168 za dhahabu, kilo 140 za fedha na mavazi ya makuhani 67.
73 Basi, makuhani, Walawi, walinzi wa hekalu, waimbaji, baadhi ya watu wengine, watumishi wa hekalu na watu wote wa Israeli, wakaishi katika miji yao.