6 Ezra akaomba kwa sala ifuatayo:“Wewe peke yako ndiwe Mwenyezi-Mungu;ndiwe uliyefanya mbingu na jeshi lake lote,dunia na vyote vilivyomo,bahari na vyote vilivyomo;nawe ndiwe unayevihifadhi hai,na jeshi lote la mbinguni lakuabudu wewe.
7 Wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu,Mungu uliyemchagua Abramu,ukamtoa toka Uri ya Wakaldayona kumpa jina Abrahamu.
8 Ukamwona kuwa yu mwadilifu mbele yako;ukafanya agano naye kuwapa wazawa wake nchi ya Wakanaani,Wahiti, Waamori, Waperizi, Wayebusi na Wagirgashi.Na ahadi yako ukaitimiza;kwani wewe u mwaminifu.
9 “Uliyaona mateso ya babu zetuwalipokuwa nchini Misri,na walipokuomba msaada kwenye Bahari ya Shamuuliwasikia.
10 Ulifanya ishara na maajabu dhidi ya Farao,watumishi wake wotena watu wote wa nchi yake;kwani ulijua kuwawaliwakandamiza babu zetu.Ukajipatia umaarufu uliopo mpaka leo.
11 Uliigawa bahari katikati mbele yao,nao wakapita katikati ya bahari,mahali pakavu.Lakini ukawatupa Wamisri waliowafuatiakama jiwe zito ndani ya maji mengi.
12 Mchana uliwaongoza kwa mnara wa wingu,na usiku uliwaongoza kwa mnara wa motoili kuwamulikia njia ya kuendea.