5 Mtu huyo, Mika, alikuwa na mahali pake pa ibada. Alitengeneza kizibao cha kuhani na kinyago, kisha akamfanya mmoja wa watoto wake kuwa kuhani wake.
6 Siku hizo hapakuwepo na mfalme katika Israeli. Kila mtu alifanya chochote alichoona ni chema.
7 Wakati huo kulikuwa na kijana mmoja Mlawi mjini Bethlehemu nchini Yuda.
8 Kijana huyo akaondoka Bethlehemu nchini Yuda, akaenda kutafuta mahali pengine pa kuishi. Katika safari yake akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya milima ya Efraimu.
9 Mika akamwuliza, “Umetoka wapi?” Naye akamjibu, “Mimi ni Mlawi, kutoka mjini Bethlehemu nchini Yuda. Nitakaa popote nitakapopata nafasi ya kukaa kama mgeni.”
10 Mika akamwambia, “Kaa pamoja nami, uwe kwangu kama baba na kuhani wangu. Nitakulipa vipande kumi vya fedha kila mwaka na mavazi pamoja na mahitaji yako.”
11 Huyo Mlawi akaingia akakubali, akakaa huko na kuwa kama mmoja wa wana wa Mika.