18 Mtu yeyote anayeua mnyama ni lazima atoe fidia: Uhai kwa uhai.
19 Mtu yeyote anayemwumiza jirani, ni lazima naye aumizwe kulingana na kiasi alichomwumiza jirani yake,
20 amemvunja mfupa naye atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kila mtu anayemwumiza mwenzake ni lazima naye aumizwe kulingana na tendo lake.
21 Anayemuua mnyama ni lazima atoe fidia; lakini mtu yeyote akimuua mtu mwingine ni lazima naye auawe.
22 Sheria hii yamhusu mgeni na mwenyeji. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”
23 Basi, Mose akawaambia Waisraeli hayo yote. Wakampeleka yule mtu aliyemlaani Mwenyezi-Mungu nje ya kambi, wakamuua kwa kumpiga mawe. Ndivyo Waisraeli walivyofanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.