27 “Na kama hata baada ya hayo yote bado hamtanisikiliza mkaendelea kunipinga,
28 basi nami nitapingana nanyi kwa hasira kali, na kuwaadhibu mimi mwenyewe mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu.
29 Ndipo mtakula watoto wenu, wa kiume na kike.
30 Nitapaharibu mahali penu pa ibada milimani, nitazibomoa madhabahu zenu za kufukizia ubani, na kuzitupa maiti zenu juu ya sanamu za miungu yenu. Roho yangu itawachukia kabisa.
31 Miji yenu nitaiteketeza mahali penu patakatifu nitapafanya jangwa na harufu zenu nzuri za sadaka kamwe sitazikubali.
32 Nitaiteketeza nchi yenu hivyo kwamba hata adui wanaohamia humo watashangaa.
33 Nitawatawanya nyinyi miongoni mwa watu wa mataifa na kuchomoa upanga dhidi yenu. Nchi yenu itakuwa ni ukiwa na miji yenu uharibifu.