1 Pigeni tarumbeta huko Siyoni;pigeni baragumu juu ya mlima mtakatifu!Tetemekeni enyi wakazi wa Yuda,maana siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja,naam, siku hiyo iko karibu!
2 Hiyo ni siku ya giza na huzuni;siku ya mawingu na giza nene.Jeshi kubwa la nzige linakaribiakama giza linalotanda milimani.Namna hiyo haijapata kuweko kamwewala haitaonekana tenakatika vizazi vyote vijavyo.
3 Kama vile moto uteketezavyojeshi hilo laharibu kila kitu mbele yakena kuacha nyuma kila kitu kinateketezwa;kabla hawajapita, nchi ni kama bustani ya Edeni,lakini wakisha pita, ni jangwa tupu.Hakuna kiwezacho kuwaepa!
4 Wanaonekana kama farasi,wanashambulia kama farasi wa vita,
5 Wanaporukaruka kwenye vilele vya milima,wanarindima kama magari ya farasi,wanavuma kama mabua makavu motoni.Wamejipanga kama jeshi kubwatayari kabisa kufanya vita.
6 Wakaribiapo, watu hujaa hofu,nyuso zao zinawaiva.