14 Huenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atabadili niana kuwapeni baraka ya mazao,mkamtolea sadaka za nafaka na kinywaji.
15 Pigeni tarumbeta huko Siyoni!Toeni amri watu wafunge;itisheni mkutano wa kidini.
16 Wakusanyeni watu wote,wawekeni watu wakfu.Waleteni wazee,wakusanyeni watoto,hata watoto wanyonyao.Bwana arusi na bibi arusina watoke vyumbani mwao.
17 Kati ya madhabahu na lango la hekalu,makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu,walie na kuomba wakisema:“Wahurumie watu wako, ee Mwenyezi-Mungu.Usiyaache mataifa mengine yatudharauna kutudhihaki yakisema,‘Yuko wapi basi Mungu wao?’”
18 Ndipo Mwenyezi-Mungu akaipenda nchi yakeakawahurumia watu wake.
19 Alisikiliza, akajibu sala zao; akasema,“Sasa nitawapeni tena nafaka,sitawafanya mdharauliwe tena na mataifa.
20 Nitawaondoa hao adui watokao kaskazini,nitawafukuza mpaka jangwani;askari wa mbele nitawatupa katika Bahari ya Chumvina wale wa nyuma katika Bahari ya Mediteranea.Watatoa uvundo na harufu mbaya,hao ambao wamefanya maovu makubwa.