5 Mmechukua fedha na dhahabu yangu, na kuvibeba vitu vyangu vya thamani hadi kwenye mahekalu yenu.
6 Mmewapeleka watu wa Yuda na Yerusalemu mbali na nchi yao, mkawauza kwa Wagiriki.
7 Sasa, nitawarudisha watu wangu kutoka huko mlikowauza. Nitawalipizeni kisasi kwa yote mliyowatendea.
8 Watoto wenu wa kiume na wa kike nitawafanya wauzwe kwa watu wa Yuda, nao watawauzia Washeba, watu wa taifa la mbali kabisa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
9 “Watangazieni watu wa mataifa jambo hili:Jitayarisheni kwa vita,waiteni mashujaa wenu;askari wote na wakusanyike,waende mbele.
10 Majembe yenu yafueni yawe mapanga,miundu yenu ya kupogolea iwe mikuki.Hata aliye dhaifu na aseme:‘Mimi pia ni shujaa’.
11 Njoni haraka, enyi mataifa yote jirani,kusanyikeni huko bondeni.”Ee Mwenyezi-Mungu!Teremsha askari wako dhidi yao!