7 Sasa, nitawarudisha watu wangu kutoka huko mlikowauza. Nitawalipizeni kisasi kwa yote mliyowatendea.
8 Watoto wenu wa kiume na wa kike nitawafanya wauzwe kwa watu wa Yuda, nao watawauzia Washeba, watu wa taifa la mbali kabisa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
9 “Watangazieni watu wa mataifa jambo hili:Jitayarisheni kwa vita,waiteni mashujaa wenu;askari wote na wakusanyike,waende mbele.
10 Majembe yenu yafueni yawe mapanga,miundu yenu ya kupogolea iwe mikuki.Hata aliye dhaifu na aseme:‘Mimi pia ni shujaa’.
11 Njoni haraka, enyi mataifa yote jirani,kusanyikeni huko bondeni.”Ee Mwenyezi-Mungu!Teremsha askari wako dhidi yao!
12 “Haya mataifa na yajiweke tayari;yaje kwenye bonde liitwalo:‘Mwenyezi-Mungu Ahukumu’.Huko, mimi Mwenyezi-Mungu,nitaketi kuyahukumu mataifa yote ya jirani.
13 Haya! Chukueni mundu wa kuvuna,kwani sasa ni wakati wa mavuno.Ingieni! Wapondeni kama zabibuambazo zimejaza shinikizo.Uovu wao umepita kiasikama mapipa yanayofurika.”