47 Watu wa kabila la Dani walipopoteza nchi yao, walikwenda na kuushambulia mji wa Leshemu. Waliushinda na kuuteka, na baada ya kuwaua wakazi wake wote, waliumiliki halafu wakabadili jina la mji huo kuwa Dani; jina ambalo lilikuwa ni la babu yao.
48 Hizo ndizo sehemu zilizopewa koo za kabila la Dani; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
49 Walipomaliza kugawiana sehemu zote za nchi, Waisraeli walimpa Yoshua, mwana wa Nuni, sehemu yake katikati yao.
50 Kulingana na amri ya Mwenyezi-Mungu walimpa mji ambao aliuchagua yeye mwenyewe, yaani Timnath-sera, ambao ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Naye Yoshua akaujenga upya mji huo na kukaa humo.
51 Basi, kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawa sehemu hizo kwa kura mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano huko Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawa nchi.