14 Kisha nikaivunja ile fimbo yangu ya pili niliyoiita “Umoja;” na hivyo nikauvunja umoja kati ya Yuda na Israeli.
15 Mwenyezi-Mungu akaniambia tena, “Jifanye tena mchungaji, lakini safari hii uwe kama mchungaji mbaya!
16 Maana nitaleta nchini mchungaji asiyemjali kondoo anayeangamia, au kumtafuta kondoo anayetangatanga, au kumtibu aliyejeruhiwa wala kumlisha aliye hai: Bali atakula wale kondoo wanono, hata kwato zao.
17 “Ole wake mchungaji mbaya,ambaye anawaacha kondoo wake!Upanga na uukate mkono wake,na jicho lake la kulia na ling'olewe!Mkono wake na udhoofike,jicho lake la kulia na lipofuke.”