10 Wazawa wa Daudi na wakazi wa mji wa Yerusalemu nitawajaza roho ya huruma na maombi, nao watamtazama yeye waliyemtoboa; watamlilia kama mtu amliliavyo mtoto wake wa pekee, au kama mtu amliliavyo kwa uchungu mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu mjini Yerusalemu kama maombolezo ya kumwombolezea Hadad-rimoni katika mbuga za Megido.
12 Nchi itaomboleza, kila ukoo utaomboleza peke yake, wanaume peke yao na wanawake peke yao; ukoo wa Daudi peke yake; ukoo wa Nathani peke yake;
13 ukoo wa Lawi peke yake na ukoo wa Shimei peke yake.
14 Jamaa zote zilizosalia zitaomboleza; wanaume peke yao na wanawake peke yao.