19 “Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema hivi: Siku za mfungo za mwezi wa nne, mwezi wa tano, mwezi wa saba na mwezi wa kumi, zitakuwa nyakati za furaha na shangwe; zitakuwa sikukuu za sherehe kwa watu wa Yuda. Basi, pendeni ukweli na amani.”
20 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Watu wengi wa mataifa ya kigeni na wakazi wa miji mingi watamiminika mjini Yerusalemu.
21 Wakazi wa mji mmoja watawaendea wakazi wa mji mwingine na kuwaambia, ‘Twendeni pamoja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wa majeshi na kumwomba baraka!’
22 Naam, mataifa yenye nguvu na watu wengi watakuja Yerusalemu kuniabudu mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi na kuniomba baraka.
23 Wakati huo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, watu kumi kutoka mataifa ya kila lugha watamng'ang'ania Myahudi mmoja na kushika nguo yake na kumwambia, ‘Tunataka kwenda pamoja nanyi, kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.’”