2 Hali kadhalika mji wa Hamathi unaopakana na Hadraki;na hata miji ya Tiro na Sidoniingawaje yajiona kuwa na hekima sana.
3 Mji wa Tiro umejijengea ngome kumbwa,umejirundikia fedha kama vumbi,na dhahabu kama takataka barabarani.
4 Lakini Bwana ataichukua mali yake yote,utajiri wake atautumbukiza baharini,na kuuteketeza mji huo kwa moto.
5 Mji wa Ashkeloni utaona hayo na kuogopa,nao mji wa Gaza utagaagaa kwa uchungu;hata Ekroni, maana tumaini lake litatoweka.Mji wa Gaza utapoteza mfalme wake,nao Ashkeloni hautakaliwa na watu.
6 Mji wa Ashdodi utakaliwa na machotara.Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kiburi cha Filistia nitakikomesha.
7 Nitawakomesha kula nyama yenye damu,na chakula ambacho ni chukizo.Mabaki watakuwa mali yangu,kama ukoo mmoja katika Yuda.Watu wa Ekroni watakuwa kama Wayebusi.
8 Mimi mwenyewe nitailinda nchi yangu,nitazuia majeshi yasipitepite humo.Hakuna mtu atakayewadhulumu tena watu wangu,maana, kwa macho yangu mwenyewe,nimeona jinsi walivyoteseka.”