36 Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru.Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha wasimwone.
37 Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini;
38 ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema,Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu;Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?
39 Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena,
40 Amewapofusha macho,Ameifanya mizito mioyo yao;Wasije wakaona kwa macho yao,Wakafahamu kwa mioyo yao,Wakaongoka, nikawaponya.
41 Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake, akataja habari zake.
42 Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi.