1 Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; na jina la mamaye aliitwa Yerusha binti Sadoki.
2 Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, sawasawa na yote aliyoyafanya Uzia babaye; isipokuwa hakuingia hekaluni mwa BWANA. Lakini watu walikuwa wakali kufanya maovu.
3 Ndiye aliyelijenga lango la juu la nyumba ya BWANA, na juu ya ukuta wa Ofeli akajenga sana.
4 Tena akajenga miji katika milima ya Yuda, na mwituni akajenga ngome na minara.