36 Kisha hao watu, ambao Musa aliwatuma waipeleleze nchi, waliorudi, na kufanya mkutano wote kumnung’unikia, kwa walivyoleta habari mbaya juu ya nchi,
37 watu hao walioileta habari mbaya ya nchi wakafa kwa tauni mbele ya BWANA.
38 Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.
39 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaombolea sana.
40 Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali BWANA alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi.
41 Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyahalifu maagizo ya BWANA? Maana halitafanikiwa jambo hilo.
42 Msikwee, kwa kuwa BWANA hamo kati yenu; msipigwe na kuangushwa mbele ya adui zenu.