16 BWANA akaonana na Balaamu akatia neno kinywani mwake, akasema, Umrudie Balaki, ukaseme hivi.
17 Akafika kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na wakuu wa Moabu pamoja naye. Balaki akamwambia, BWANA amenena nini?
18 Naye akatunga mithali yake, akasema,Ondoka Balaki, ukasikilize;Nisikilize, Ee mwana wa Sipori;
19 Mungu si mtu, aseme uongo;Wala si mwanadamu, ajute;Iwapo amesema, hatalitenda?Iwapo amenena, hatalifikiliza?
20 Tazama, nimepewa amri kubariki,Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua.
21 Hakutazama uovu katika Yakobo,Wala hakuona ukaidi katika Israeli.BWANA, Mungu wake, yu pamoja naye,Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao.
22 Mungu amewaleta kutoka Misri,Naye ana nguvu kama nguvu za nyati.