2 Balaki akafanya kama Balaamu alivyonena. Balaki na Balaamu wakatoa sadaka, ng’ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu.
3 Balaamu akamwambia Balaki, Simama karibu na sadaka yako, nami nitakwenda, labda BWANA atakuja kuonana nami; na lo lote atakalonionyesha nitakuambia. Akaenda hata mahali peupe juu ya kilima.
4 Mungu akakutana na Balaamu; naye Balaamu akamwambia, Nimetengeneza madhabahu saba, nami nimetoa sadaka ng’ombe mume mmoja na kondoo mume mmoja juu ya kila madhabahu.
5 BWANA akatia neno katika kinywa chake Balaamu, akasema, Umrudie Balaki; ukaseme maneno haya.
6 Akarudi kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, yeye na wakuu wote wa Moabu pamoja naye.
7 Akatunga mithali yake, akasema,Balaki amenileta kutoka Aramu,Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki,Njoo! Unilaanie Yakobo,Njoo! Unishutumie Israeli.
8 Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani?Nimshutumuje, yeye ambaye BWANA hakumshutumu?